Waziri wa Habari Utalii na Mamboyakale Mh. Mahmoud Thabit Kombo ameupongeza Uongozi wa Hoteli ya Melia kwa kunyakua tuzo ya upatikanaji wa Huduma bora katika Hoteli hiyo.

Mh. Mahmoud ametoa pongezi hizo za dhati katika ghafla maalumu yakusherehekea tuzo hiyo huko Hoteli ya Melia Kiwengwa Kaskazini B Unguja.

Amesema miongoni mwa ahadi zilizopo katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kushirikiana bega kwa bega pamoja na Sekta binafi zinazojihusisha na harakati za Utalii kwahiyo hakuna budi kuungana kwa pamoja ili kusherehekea tuzo kama hizo.

Mbali na hayo pia amewataka Waandishi wa Habari Zanzibar kuendelea kuitangaza Sekta ya Utalii kwani chombo cha Habari ndio njia mojawapo inayofanya kazi ya kuiendeleza na kuikuza sekta hiyo.”Kazi yenu ni kupiga kampeni hivyo basi tumieni fursazenu katika kuhabarisha,nahata wananchi  kuwajuulisha kiundani vivutio viliopo nchini wavijue”amesema Mh. Mahmoud

Nae Mkuu wa wafanyakazi katika Hoteli hiyo Bi Sabra Omar amesema siomara ya kwanza kupata tuzo kama hiyo napia wamefurahika zaidi kuona tuzo kama hizo zinajitokeza hoteli hiyo kila mara.

Tuzo ya hiyo waliyoipata Melia ni tuzo bora kwa kuibuka mshindi katika hoteli inayotoa huduma nzuri ambayo inaongoza kwa ubora Afrika nzima pamoja na Bahari Hindi.

Ndani ya Zanzibar kwa mwaka 2019 umefanikiwa kupokea tuzo tofauti  ikiwemo tuzo ya Egypt, Chumbe Island  Essque Zalu na Melia.