Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya kale Mh. Mahmoud Thabit Kombo kulia akiwa na kiongozi wa hoteli ya ESSQUE ZALU Cyrus Mutuota katika hafla ya kusherehekea tuzo huko Nungwi ESSQUE ZALU Kaskazini Unguja.

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya kale Mh. Mahmoud Thabit Kombo amewataka Waandishi wa Habari Zanzibar kuendelea kushirikiana kwa moyo mmoja na Sekta ya Utalii ili kuendeleza kutoa taarifa kwa umma zinzohusiana na Utalii ili Uchumi wa nchi uzidi kukua.

Waziri Mahmoud ameyasema hayo katika sherehe ya kusherehekea kwa upatikanaji wa tunzo bora  walizozipata Uongozi wa Hoteli ya ESSQUE ZALU ikiwa moja tunzo ya utekelezaji bora wa huduma kwa Zanzibar( Zanzibar leading Hotel 2019) na yapili kwa Tanzania (Tanzania’s Leading Hotel 2019)

Amesema waandishi wamekua wakifanya kazi nzuri pamoja na jitihada kubwa katika sekta ya Utalii hivyo nivizuri kuengeza kasi zaidi kwa lengo la kuleta maendeleo nchini.

Hata hivyo ameupongeza uongozi wa Essque Zalu Hotel kwa kupata zawadi hiyo na amewataka wale wote ambao wanajishuhulisha na shuhuli za Utalii kuwa milango ya Kamisheni ya Utalii ipo wazi na imejiandaa kwa kina kwaajili ya usajili.

 Amesema yoyote atakaeshida tuzo kama hizo basi Wizara ya Habari hainabudi kuwajibika kumpongeza“Tutatoka siisi Wizarani kuenda kwake kwa sababu mtu huyo atakua ameongeza nyota nyengine yasifa na kivutio katika nchi yetu ya Zanzibar”

“Tuna Hoteli pamoja na nyumba za kulala 476 zilizosajiliwa na Kamisheni ya Utalii Zanzibar na vitanda zaidi ya  elfu nane vyakulala na kwa yule yoyote atakae shinda atakua ameongezewa nyota kama wanavyo engezewa nyota wanajeshi kwenye mabega na tutatoka sisi kwaniaba ya Serikali kwenda kumpongeza kwasababu atakua ameiongezea nyota nasifa Zanzibar” amesema  Waziri Mahmoud

Wakati huo huo akizungumza na waandishi wa Habari kiongozi wa hoteli hiyo Cyrus Mutuota ametoa wito kwa Serikali kuwa pamoja nao katika kuwapa elimu vijana inayohusiana na utalii kwani katika Hoteli wanahitajika wale ambao wamesomea vyema elimuhiyo.

Essque Zalu imepokea tunzo hizo mnamo tarehe 1 mwezi wa 6 2019 huko Mauritius ambapo Ndani ya Zanzibar kwa mwaka 2019 umefanikiwa kupokea tuzo tofauti  ikiwemo tuzo ya Egypt, Chumbe Island na Essque Zalu.