Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemtaka  Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani(Profesa Majimarefu) kuwa subra katika kipindi hichi ambacho anaumwa na kumtaka azidishe maombi ili warudi kuungana pamoja kwa ajili ya kuitumikia jamii.

Mbunge huyo ambae pia ni mtaalamu wa tiba asilia amelazwa katika hospitali ya Kairuki, Mikocheni jijini Dar es salaam ambako waziri Majaliwa alikwenda kumtembelea.