Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kuacha kutoa taarifa za ugonjwa CORONA, kwani Taarifa zote za ugonjwa huu zitatolewa na Waziri wa Afya, kama ni łazima atatoa Waziri Mkuu, kama ni lazima sana atatoa Makamu wa Rais au Rais mwenyewe.

Kauli hiyo ameisema leo wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ambayo imepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Natambua mchango wa kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), juu ya watu kutoa taarifa (za ugonjwa wa Corona) kiholela. Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya kila mmoja anatamka anavyotaka” amesema Waziri mkuu