Waziri wa Afya wa Austria, Rudolf Anschober mwenye umri wa miaka (60) ametangaza kuachia wadhifa huo kwasababu ya uchovu, akisema miezi 15 aliyokuwa ofisini imeonekana kama miaka 15.

Anschober aliteuliwa Januari mwaka 2020 na kuongoza Taifa hilo katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona amesema Taifa linahitaji Waziri wa Afya ambaye yupo imara kwa asilimia 100.

Amesema amekuwa akifanya kazi kupitiliza na amechoka, pia amekuwa na changamoto kadhaa za kiafya ikiwemo Shinikizo la Damu.