Wadudu wanaosababisha ugonjwa wa kipindupindu wapunguwa Zanzibar kutoka elfu moja hadi kufikia 50 (hamsini)…

Waziri wa afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amesema mbali na kupunguwa kwa kasi ya maambukizi ya maradhi ya kipindupindu Zanzibar wananchi wanajukumu la kuendelea kutunza mazingira  ili kutokomeza maradhi hayo nchini.

DSC_0176

Akizungumza katika ghafla ya kutembelea kambi ya wagonjwa wa kipindupindu  chumbuni amesema mbali na kambi za kupindupindu kufungwa kutokana na ugojwa huo kupunguwa lakini bado wananchi wanajukumu la kufuata masharti ya kiafya hususani kwa wafanyabiashara kutokana na  mdudu wa maradhi ya kipindupindu kuendelea kuwepo kisiwani zanzibar.

DSC_0228

Aidha amesema katika kuwajali wafanyabiashara nchini ametowa wito kwa wanafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama mama lishe na baba lishe kujitokeza katika kupima afya zao kwa lengo la kuendelea na kufanya biashara zao.

Wakati huo huo Muwakilishi kutoka shirika la afya duniani  (WHO) Rufaro Chatora  ameiomba serikali ya Zanzibar kulitilia mkazo suala ya usafi wa mazingira  kwa wananchi ikiwemo kukosha mikono yao wakati wa kula pamoja na kutumia vyoo katika makaazi yao ili kunusuru kasi ya maradhi ya mripuko kurejea nchini.

Kwa mujibu wa tathmini ya shirika la afya duniani (WHO) ugonjwa wa kipindupindu umeathiri sehemu ya Tanzania na kupelekea watu 22,279 kuugua ugonjwa huo na wagonjwa 345 kufariki dunia wakati Zanzibar wagonjwa waliuguwa 4,326 kati yao 68 kufariki dunia.