Serikali ya Mapinduzi ya zanzibar imesema kuchelewa kufanya Biashara kwa wapangaji wa Maduka ya jengo la Treni darajani kumesababishwa na baadhi ya kukosa sifa za kuendelea na Biashara ikiwemo baadhi yao kukosa leseni.

Akijibu swali katika mkutano wa baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar,Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk.khalid Salum amesema lengo la serikali ni kuona wafanya Biashara wanaendelea na Biashara zao ili wajikwamue na ugumu wa maisha.

Amesema sababu nyengine za kuchelewa kufunguliwa kwa maduka hayo ni Wapangaji hao kushindwa kuwasilisha Rikodi na taarifa Muhimu za kufanyia baishara zao.

Dk,Khalid amesema pia kumejitokeza kesi kwa baadhi ya Wapangaji hao maduka yao kumilikiwa na familia au Mpangaji zaidi ya Mmoja pamoja na Wafanya biashara kuwa na Mikataba isiyokuwa  ya kwao jambo ambalo linachelewesha ukusanyaji wa taarifa muhimu.

Akizungumzia tatizo la bei linalodaiwa kupanda kwa maduka hayo amesema hakuna bei kubwa wanazotozwa wafanya biashara hao na bei iliopo inaendana na Wapangaji hao kulingana na sehemu wanazotaka.

Waziri khalid amesema mpaka sasa tayari kuna baadhi ya wafanya biashara wameshamaliza taratibu zinazohitajika na wanatarajia kuanza kufanya kazi mda wowote kuazia sasa.

Amesema Mfuko wa hifadhi ya jamii zanzibar ZSSSF inaendelea na uataratibu wake wa kuwapa kiumbele Wapangaji waliokuwepo awali katika eneo hilo ili waweze kuendelea na Biashara zao baada ya kukamilisha taratibu zinazohitajika.