Mkurugenzi wa mashtaka Kenya ameagiza kukamatwa kwa waziri wa fedha Henry Rotich na ashtakiwe kuhusu ufisadi

Mkurugenzi huyo wa mashtaka Noordin Haji amekuwa akizungumza katika vyombo vya habari kuhusu uamuzi wa kumshtaki waziri wa fedha Kenya Henry Rotich, na maafisa wengine wa serikali kuhusu kandarasi zilizotolewa kwa kampuni ya Italia kujenga mabwawa mawili.

Waziri huyo wa Fedha na maafisa wengine kadhaa wanatarajiwa kukamtwa muda wowowte kuanzia sasa baada ya Haji kuwatuhumu kuhusuika katika ufisadi.

Noordin Haji ameeleza kwamba watashatakiwa kwa “kupanga kufanya udanganyifu, kushindwa kutii muongozo unaotumika katika upatikanaji wa kandarasi” miongoni mwa mambo mengine.

Mashtaka hayo yanahusiana na ujenzi wa mabwawa mawili nchini uliogharimu fedha nyingi.

DPP NOORDIN HAJJI

Mnamo Machi Waziri Rotich alikana kupitia tangazo kubwa kwenye gazeti nchini kufanya makosa yoyote.

Kampuni hiyo ya Italia CMC de Ravenna pia imekana tuhuma hizo.

“Katiba yetu inasisitiza baadhi ya maadili yetu yakiwemo uadilifu… kuyatimiza hususan kwa walio uongozini…”

DPP Noordin Haji directs for arrest & prosecution of Treasury CS Henry Rotich, PS Kamau Thugge, PS EAC Susan Koech, KVDA MD David Kimosop, CEO NEMA Geoffrey Wahungu & 23 others over Sh 63 Billion Arror & Kimwarer Dams scam.— ODPP_KE (@ODPP_KE)

“Kutimizi maadili haya ni muhimu kwa uhai wetu…’ amefafanua mkurugenzi huyo wa mashtaka.

“Rushwa inatishia msingi wa taifa letu – ufisadi unatugawanya na kuangamiza utu..”

Rushwa inatishia msingi wa taifa letu – ufisadi unatugawanya na kuangamiza utu…Noordin Hajji , Mkurugenzi wa mashtaka Kenya

“Kila kesi inatuma ujumbe mzito kwa walio wafisadi … au kwa wanoavutiwa kuingia katika ufisadi… kwamba watashtakiwa…”

Haji ameeleza kwamba kashfa kuhusu ujenzi wa mabwawa hayo umewagharimu Wakenya walipoa kodi mabilioni ya fedha katika malipo yanayotiliwa shaka.

Maafisa wengine walioagizwa kukamatwana kushtakiwa ni pamoja na katibu mkuu katika wizara ya fedha Kamau Thugge, Dkt Susan Jemutai Koech kutoka wizara ya jumuiya ya Afrika mashariki na mkurugenzi msimamizi wa mamlaka ya maendeoe ya Kerio Valley (KVDA) David Kimosop.

Taarifa kuhusu gharama ya ujenzi wa mabwawa hayo ziligubika mijadala katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini mnamo Machi mwaka huu.

Mamlaka ya Kerio Valley Development Authority (KVDA) ilitoka wazi na kujaribu kuzima tuhuma kwamba imeilipa kampuni ya hiyo ya Italia shilingi bilioni 21 za Kenya na kufafanua kwamba ni shilingi bilioni 7.6 pekee.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, KVDA ilisema mkandarasi huyo – CMC Di Ravenna – alilipwa kwa mafungu mawili kujenga mabwawa hayo ya Arror na Kimwarer katika kaunti ya Elgeyo Marakwet Kaskazini mwa Kenya.

Akizungumzia kuhusu uchunguzi kuhusu namna kandarasi za ujenzi wa mabwawa hayo zilizvyotolewa, Mkurugenzi wa mashtaka Kenya Noordin amesema:

“Imebainika kwamba namna mpango ulivyoidhinishwa, ulivyo patikana na malipo yalivyotolewa kwa mradi wa mabwawa hayo, umegubikwa kwa ukiukaji mkubwa wa sheria.”