Waziri wa mambo ya kigeni wa Pakistan aizuru India kujadili jimbo la Kashmir Waziri wa mambo ya kigeni wa Pakistan Shah Mahmood Qureshi, anatarajiwa kuelekea China kama sehemu ya juhudi za kuishinikiza India kubadilisha uamuzi wake wa kufuta hadhi maalum ya jimbo linalogombaniwa la Kashmir.

Mahmood Qureshi atakutana na viongozi wa China hii leo Ijumaa Kabla ya kuondoka kuelekea Beijing Qureshi, alisema atazungumza na mshirika au rafiki wa India ambaye ni China kuhusu hali ilivyo baada ya taifa hilo kushusha hadhi ya sehemu ya jimbo la Kashmir kutoka kuwa taifa hadi jimbo na kudhibiti uwezo wake wa kufanya maamuzi, pamoja na kuliondolea haki yake ya kikatiba.

Jimbo linalodhibitiwa na India Kashmir limekuwa chini ya ulinzi mkali kuzuwiya machafuko tangu uamuzi huo ulipotangazwa. Jimbo hilo linalogombaniwa na Pakistan na India limegawika kati ya mataifa hayo mawili. Pakistan hata hivyo imesema inafikiria pendekezo la kufika katika mahakama ya kimataifa ya sheria juu ya uamuzi wa India.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Pakistan Shah Mahmood Qureshi, anatarajiwa kuelekea China kama sehemu ya juhudi za kuishinikiza India kubadilisha uamuzi wake wa kufuta hadhi maalum ya jimbo linalogombaniwa la Kashmir.

Mahmood Qureshi atakutana na viongozi wa China hii leo Ijumaa. Kabla ya kuondoka kuelekea Beijing Qureshi, alisema atazungumza na mshirika au rafiki wa India ambaye ni China kuhusu hali ilivyo baada ya taifa hilo kushusha hadhi ya sehemu ya jimbo la Kashmir kutoka kuwa taifa hadi jimbo na kudhibiti uwezo wake wa kufanya maamuzi, pamoja na kuliondolea haki yake ya kikatiba.