Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Leo April 6, 2020, ataanza rasmi zoezi la kuwakamata wazururaji wote wa Mkoa huo, wanaoingia mjini bila ya kuwa na kazi yoyote ikiwa ni tahadhari ya Virusi vya Corona.

“Umuhimu wa kuchapa kazi uko palepale, kuanzia Jumatatu tutakamata wazururaji wote mjini wasiokuwa na kazi ya maana, hao ndiyo wanaosababisha mikusanyiko isiyokuwa na tija, unaenda stendi, Sokoni, Bandarini huna kazi huo ni uzururaji unahatarisha maisha ya watu wengine” amesema Rc Makonda.