Wema Sepetu afunguka kuwa na mahusiano na mwanaume mpigaji

Malkia wa filamu Bongo Wema Sepetu amefunguka atakavyomchukulia mwanaume anayepiga iwapo atakuwa nae katika mahusiano ya kimapenzi.

Katika sherehe ya kuzaliwa ya meneja wake, Neema Ndepanya  iliyofanyika nyumbani kwa Wema, Salasala jijini Dar es Salaam, Wema Sepetu alisema katika maisha ya uhusiano, anafurahia kuwa na mwanaume ambaye atampa kipigo kidogo pale anapokosea.

Wema Sepetu ametoa kauli hiyo baada ya kuulizwa na Ijumaa Wikienda kuhusu aina ya mwanaume anayependa kuwa naye, ndipo alipotoa ya moyoni.“Napenda mwanaume anipe kipigo kidogo siyo mwanaume mnaishi miaka yote, halafu hata kukupiga kofi kidogo hakupigi,” alisema Wema.