Wema Sepetu amuonesha Mume mtarajiwa wakiwa Kitandani, arusha kijembe

Tanzania Sweatheart, Miss Tanzania 2006 na Mrembo asiyepungua umaarufu wake Wema Sepetu ameusimamisha mtandao wa Internet dakika chache zilizopita baada ya kumuweka hadharani mume wake mtarajiwa wakiwa katika picha ya faragha.

Wema ameweka picha hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akionesha kujihami kwa kuzuia mashabiki wake kuandika chochote kwenye picha.

Baada ya kuweka picha hiyo Wema, ametumia ukurasa wake huohuo kuwataka mashabiki wake na watu wote kwa ujumla kushughulikia maisha yao.

Wema Sepetu anaendelea kuwa ni mmoja wa watu maarufu anaeongelewa sana kwa kipindi cha miaka 12 mfulululizo huku mahusiano yake ya kimapenzi ikiwa ni moja ya jambo linalozungumzwa zaidi.