Kesi ya liyekuwa Miss Tanzania 2006 na msanii wa filamu za Bongo, Wema Sepetu inayomkabili, ya kusambaza video zenye maudhui ya ngono kupitia ukurasa wake wa Instagram Oktoba 15, mwaka jana imesikilizwa tena leo mahakama ya hakimu mkazi kisutu, Dar es Salaam.

Wema Sepetu apewa onyo na Mahakama hiyo baada ya kukiuka masharti ya dhamana yake, hata hivyo ameachiwa kwa dhamana na kesi yake itasikilizwa tena July 4 mwaka huu.

Utakumbuka June 24 mwaka huu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamuru msanii huyo kwenda jela hadi siku ya leo kusubiria uamuzi wa mahakama wa kumfutia dhamana.