Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema majaribio yanayofanyiwa dawa ya ugonjwa wa malaria Hydroxychloroquine ili kuona iwapo inaweza kutibu virusi vya Corona yamesitishwa kutokana na hofu ya usalama wake.

Vipimo vilivyokuwa vikifanywa katika mataifa kadhaa vimesitishwa kwa muda kama hatua ya kuchukua tahadhari, Hatua hiyo inajiri baada ya utafiti wa tiba uliofanyika hivi karibuni kusema kwamba dawa hiyo inaweza kuongeza hatari ya mgonjwa kufariki kutokana na virusi hivyo.

Wakati WHO ikisitisha dawa hiyo, Rais wa Marekani Donald Trump yeye amesema kuwa anatumia dawa hiyo kuzuia virusi hivyo.