Wizara ya Afya Zanzibar imesema hatua ya awali ya zoezi la kurekebisha mipaka, uwekaji wa bikon pamoja na nguzo katika eneo la Binguni linalotarajiwa kujengwa Hospital mpya na ya kisasa umekamilika.

Akizungumza katika eneo hilo la binguni mara baada ya kukagua eneo hilo Naibu Katibu Mkuu wizara ya afya zanzibar ndugu Halima maulid salum amesema hatua iliyofikiwa ni nzuri licha ya kuwa na kasoro ndogo ndogo zinazohitaji kufanyiwa marekebisho kwani limeweza kumalizika kwa wakati uliopangwa.

Amesema uwepo wa mashirikiano ya karibu kwa Taasisi zinazohusika zimeweza kufanikisha zoezi hilo kwa wakati uliopangwa na kusisitiza umuhimu wa kuendelezwa mashirikiano yaliyopo ili kutimiza azma ya serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Nae sheha wa hehia hio ali Yussuf Mussa amesema wananchi ambao wanaishi na wanaojenga ndani ya eneo hilo lilipimwa wamekuwa na hofu kubwa ya kutaka kujua juu ya hatma yao ya maisha.

Akizungumzia kuhusu suala la hatma ya wananchi ambao nyumba zao zimo ndani ya mipaka ya eneo hilo mkuu wa mkoa kusini unguja mhe Hassan Khatib Hassan amewataka wananchi kuwa watulivu na kutokuwa na hofu pia kutoendelea na ujenzi wa aina yoyote katika maeneo hayo hadi pale Serikali itakapotoa maelekezo.

Ziara hiyo pia ilihudhuriwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo ambapo wamewataka wananchi kuyalinda maeneo hayo na kuacha tabia za kuzing’oa alama za mipaka zilizowekwa.