Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar, imetangaza kuzifunga skuli zote z a serikali na binafsi kuanzia leo jumatano tarehe 10 mei hadi wizara itakapo tangaza tena kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika visiwa vya Unguja na pemba.

Aidha Wizara ya Elimu imesema kuwa tangazo hili haliwahusu wanafunzi wanaondelea kufanya mitihani ya kidato cha sita, wao wataendelea kwenda skuli kama Kawaida.