Yanayofanywa na kamati teule ya ZFA ni mfano wa uongozi wa michezo

Kamati iliyoteuliwa na mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar imekuwa ikiendelea na majukum yake ya kila siku ya kuusimamia ligi kuu ya Zanzibar na mashindano ya mabingwa ya wilaya na upatikanaji wa Katiba mpya ya ZFA.

Kwasasa kamati teule imeshatoa rasimu ya kanuni ya mashindano ya msimu wa mwaka2018/2019 ili kuendesha mashindano hayo ya msimu ujao kwa kundosha maneno na lawama kwa wachezaji na viongozi hata wadau wa nje ya mpira yaani wapenzi.

Moja ya jambo kubwa lilofanywa na kamati teule ni kusimamia kanuni kuondosha ubabaishaji kwa vilabu na wachezaji wasio na nidhamu ya mpira kwa kupewa adhabu bila ya kumuangalia mtu usoni au kuoneana haya.

Tunaipongeza sana kamati ya ZFA sisi Zanzibar24 kwa kuwa imekuwa kero kwa muda mrefu kwenye soka la Zanzibar kuwa na viongozi wanaoendekeza muhali na kuona haya katika kusimamia mpira wa Zanzibar na matokeo yake kuvurigika kwa haiba ya mpira wa Zanzibar.

Matukio yaliyofanywa na kamati kipindi hichi kama vile kuvifungia vilabu vine vya kundi A, katika  mashindano ya vilabu bingwa wilaya na kuvipiga faini na kuipiga faini klabu ya Gullioni FC na kuwafungia wachezaji wake wawili ni moja ya chachu ya kuona tunakwenda kujenga mpira wa Zanzibar huku tukisubiri nani atapewa dhamana ya kuusimamia mpira wa Zanzibar.

Upangaji matokeo moja tatizo kubwa kwenye soka la Zanzibar kwa kuwa limekuwa likivuma kwa lawama kwa viongozi wa vilabu na wachezaji wenyewe hufanya mpira wa Zanzibar ulojaa vipaji na wachezaji wenye viwango vya kisasa kuonekana hauna thamani.

Yako makundi ndani ya Zanzibar na nje ya Zanzibar hayaungi mkono jitihada za kamati  kwa sababu zao binafsi kwa kuwa kipindi cha vingozi wa awali labda walikuwa wakipeleka rushwa na timu zao kutengenezewa nafasi ,wengine walikuwa wakifaidika na viongozi walio pita kwa maslahi binafsi hivyo anapotokea mtu kuziba pengo hili ni wazi unaona jinsi kamati inavyosemwa.

Sasa kamati inaendelea na majukumu yake ni kazi ya wadau wa mpira wa miguu Zanzibar kuisadia kamati hata kwa ushauri kwa lengo la kujenga mpira wa Zanzibar huku tukisubiri nani atakuja kupewa dhamana ya kuongoza mpira wa Zanzibar katika uchaguzi wa ZFA.

 Na: IBRAHIM MAKAME  ZANZIBAR24