Yanga bado haijamalizana na Reuben Bomba

Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, umesema bado haujamalizana na straika Reuben Bomba.

Licha ya jana kutoka taarifa kuwa tayari imeshamalizana naye kwa kila kitu, Nyika ameibuka na kueleza bado hajasaini mkataba wowote.

Nyika amesema endapo mchezaji huyo atakamilisha taratibu zote na akishasaini wataliweka wazi ili kila mdau, shabiki na wanachama wa Yanga aweze kufahamu.

“Bado hatujamalizana na Bomba, nadhani wakati ukishafika tutatangaza akishakamilisha kila kitu, kwa sasa bado hajasamwaga wino” alisema.

Wakati huo kikosi cha Yanga kinajiwinda na mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United utakaoipigwa mwishoni mwa wikiendi hii.