Vinara wa Ligi Kuu Soka Tanzania bara timu ya Yanga Sc mpaka sasa imeweka rikodi ya kutoruhusu kufungwa hata goli 1 katika Mashindano ya Kombe la Mapinduzi Cup yanayoendelea Visiwani Zanzibar.

Katika Michezo 2 iliyocheza Yanga Sc walitoka sare ya 0-0 mbele ya Jamhuri kisha kuwafunga bao 1-0 Namungo, ambapo Yanga Sc ndio timu pekee msimu huu katika Mashindano ya Mapinduzi Cup kumaliza dakika 180 (michezo 2) pasipo kuruhusu lango lake kufungwa.

Mashindano hayo yalioshiriki timu 9 mwaka huu timu zote 8 zimeruhusu lango lao kufungwa ila isipokuwa Yanga pekee.