Yanga yawaacha Ajib na Makambo kombe la Mapinduzi

Kuelekea michuano ya kombe la Mapinduzi inayoanza kesho Januari 1, 2019 visiwani Zanzibar, klabu ya Yanga haitapeleka kikosi chake cha kwanza kwenye mashindano hayo.

Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya Yanga kimeeleza kuwa baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza wamepewa mapumziko na kocha Mwinyi Zahera ili kujiweka sawa kwaajili ya mechi za ligi kuu.

”Badala ya kwenda na kikosi cha kwanza mwalimu ameeleza kuwa Yanga itakwenda na wachezaji ambao wamekuwa hawapati nafasi ili nao waweze kucheza na kujenga uwezo wa kujiamini’‘, kimeeleza chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa.

Miongoni mwa wachezaji ambao hawatakwenda ni kinara wa mabao wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu, Heritier Makambo, pamoja na Ibrahim Ajib na wachezaji wengine.

Katika michuano hiyo ambayo inatarajiwa kufikia tamati Januari 13, Yanga imepangwa kwenye Kundi B na timu za KVZ, Malindi, Jamhuri, Azam na Yanga.