Msanii wa muziki wa Hiphop nchini Young Killer amefunguka na kusema kuwa sababu iliyompelekea kuondoka katika music label ya Wanene ni kuisha kwa mkataba Wake wa miezi Sita.

Young Killer ameweka wazi kuwa baada ya kuisha kwa mkataba Wake hakutaka kusaini tena na label hiyo kwa sababu kwa muda ambao amefanya nao kazi kuna matarajio aliyategemea ndani ya kampuni hiyo lakini hakufanikiwa kupata alichokuwa anatafuta na kwamba badala yake aliona ni bora alipokuwa anafanya kazi akiwa mwenyewe.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Young Killer aliweka wazi kuwa moja kati ya mambo aliyokuwa anayatarajia lakini hakuyaoni ni pamoja na kukuza wigo wa muziki wake nje ya mipaka ya Tanzania.

Unajua hakuna kitu kizuri katika muziki wetu kama mafanikio ya kuzidi kupata connection tofauti-tofauti. Pia, nilikuwa nategemea kuona nyimbo zangu hata zinapigwa ‘Trace’, ili kuleta utofauti wa Young Killer yule ambaye alikuwa anafanya kazi mwenyewe na huyu ambaye anafanya kazi na Menejimenti kubwa kama Wanene.

Hiyo ni moja ya mambo, lakini vitu ni vingi“. Young Killer amesema pamoja na kuondoka katika label hiyo yupo tayari kufanya kazi na label nyingine endapo tu atapendezwa na mkataba atakaopewa.