Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Tanzania Young Killer Msodoki amesema wanafuatilia kazi zake wasipende kumpangia au kuingilia ni jinsi gani aanze kuishi na yeye anaamini anachokifanya kiko sawa.

Killer amesema hayo wakati akifanya mazungumzo na Refresh ya Wasafi Tv ambapo alisema  kwenye Muziki hakuna aliyemshauri aingie kwenye Tasnia hiyo na hata sasa basi watu wasiweke maneno maneno afanye kitu gani hususani swala la Fashion kwa kuwa Hata nywele zake haziimbi anayeimba ni yeye na anaamini anaburudisha.