Chama cha mchezo mpira wa meza Zanzibar (Z T T A) kinaendelea na mandalizi ya mashindano ya Afrika Mashariki nchini Rwanda mwezi huu kuanzia tarehe 10.

Akizugumza na Zanzibar24 Katibu wa chama hicho Ahmedi Abdalla Mussa amesema baada ya kumaliza mashindano ya UMISETA kule mwanza sasa wao kama chama chini ya Idara ya Elimu,michezo na Utamaduni wanajiandaa na mashindano hayo makubwa Afrika Mashariki na kati.

Aidha Ahemed amesema mandalizi ya awali ya tayari na wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Skuli ya Haile Salisie mjini Unguja ili kuleta ushindani katika mashindano hayo wao ndio wenye wasimamizi wa mchezo huo

Kwa upande mwengine Ahmedi amewashukuru idara ya Elimu,Michezo na Utamaduni kupitia wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kugharamia safari za wachezaji wao na msafara mzima wa utakao kwenda Rwanda kwenye mashindano hayo.

“sisi ndio walezi tunatarajia kuelekea kwenye mashindano hayo na vijana wetu 4 ambao ndio walichukua Ushindi kwenye mashindano ya Umiseta kule mwanza hawa ndio watakao shiriki mashindano hayo”Alifafanua Ahmedi .

Kwa upande mwengine Ahmedi ameelezea mikakati ya chama cha mpira wa meza Zanzibar ni kuwa na wachezaji wengi na walimu wengi wa mchezo huo kwa upande wa Skuli zote za Unguja na Pemba ili kuweza kutoa ushindani katika mashindano mbali mbali ya kimataifa.

“Tumekuwa na mpango maalum kwa walimu wote wanaofundisha mchezo huu kila siku ya Jumamosi na jumapili kukutana kufundishana kozi ndogo ndogo na mabadiliko ya sheria ya mchezo huu ili kuona tunapiga hatua na kuwa na ligi bora ya Zanzibar ya meza” Alisema Ahmedi.

Chama cha mpira wa meza Zanzibar ni moja ya vyama vinavyongozwa na viongozi wapya na tayari wanatarajia kuwakilisha kwenye mashindano ya Afrika Mashariki mwezi huu badala ya UMISETA ya Mwanza kuchukua nafasi ya kwanza kwa kanda ya Zanzibar.