ZABA yakabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ufugaji nyuki

Jumuiya ya ufugaji nyuki (ZABA) Octoba 7/ 2018 imekabidhi vyeti kwa wanafunzi walioshiriki katika mafunzo ya ufugaji nyuki huko Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.

Akizunguza ndani ya hafla hiyo Mgeni Rasmi wa shuhuli hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mh. Hassan Khatibu Haji amewataka wale wote waliobahatika kupata vyeti hivyo lazima wapambane na ujasiri wa kuzalisha zao hilo na pia kuithamini kazi yao kibiashara zaidi ili waweze kuendelea kimaisha.

Kwaupande wake Afsa Nyuki Idara ya Misitu Mali asili zisizorejesheka Bi Mwajuma Hajji Ussi amesema endapo ufugaji wa nyuki utaendeleo ipasavyo itapelekea uhifadhi bora wa misitu kwa mazingira ya visiwa vya Zanzibar.

Akisoma Risala miongoni mwa wanafunzi hao ameeleza changamoto iliopo  ndani ya ufugaji wa nyuki ni ughali wa vifaa vinavyohitajika katika ufugaji huo na kuiomba Serikalikushirikiana nao katika suala hilo ili kuweza kujikwamua na hali duni ya maisha.

Vyeti hivyo vimetolewa kwa wahitimu 67 wakiwemo wanaume 28 na wanawake 39 kutoka Shehia tatu za Wilaya ya Kusini ikiwemo Paje,Muyuni C, na Kizimkazi Mkunguni na kila kikundi kilijifunza kwa muda wa miezi sita.

Mafunzo hayo yalijumuisha mambo mbali mbali ikiwemo utunzaji wa nyuki, elimu ya mizinga, ufugaji w anyuki, ukamataji wa nyuki,uvunaji wa mazao ya nyuki pamoja na masoko.