Mamlaka  ya kupambana na kuzuiya rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar Zaeca kitengo cha madawa ya kulevya kimewakamata watu watatu kwa tuhuma  ya  kukutwa na madawa ya kulevya katika maeneo tofauti.

Akizungumza na Zanzibar24  Afisa Habari wa Mamlaka hiyo Mwanaidi Suleiman amesema  zaeca  kupitia kitengo hicho ilifanya msako maalumu na kufanikiwa  kuwakamata  watu hao  katika eneo la kianga, kwarara na kilimani Mjini unguja ambapo kesi hiyo  tayari imesha kamilika  uchunguzi wake na hatua inayofata sasa ni kuwafikisha katika ofisi ya DDP ili kupelekwa mahakamani.

Akiwataja watu hao ni Faustian Amiri Salum mwenye umri wa miaka 42 amekamatwa na mafurushi 40 ya bangi ,Ismail Haji Habibu mwenye umri wa miaka 20 amekutwa na kete  250 za unga aina ya heroin  na Mussa Shabani ambae amekutwa na kete 19 za madawa ya kulevya aina ya heroin.

Aidha Mwanaidi amewataka wananchi kuzidisha mashirikiano  katika kuwafichua  wasambazaji wa madawa ya kulevya nchini  ili kupunguza  ongezeko la watumiaji wa dawa hizo.

Amina Omar