Shirikisho la vyuo vikuu na Elimu ya juu Zanzibar (ZAHLIFE) limefanya maboresho ya kanuni zake za michezo baada ya kuagizwa na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kupitia kitengo cha Elimu na michezo .

Akizugumza na Gazeti hili Katibu wa kamati ya Elimu,habari na michezo Masudi Juma amesema wao wamelipokea agizo hilo baada ya malalamiko ya muda mrefu kwa baadhi ya vyuo pale wanapondesha mashindano yao hivyo wizara ikaamua kututaka kubadilisha kanuni zetu za mashindano ya ndani.

Masudi Juma amesema kanuni zao za mwanzo hazikuwa bora zilikuwa na utata hivyo wakaamua kubadilisha kanuni ya mpira wa miguu kabla ya michezo mengine midogo kufanyiwa marekebisho tofauti ,na pia amedai kwa sasa wanatarajia kuwa na kalenda maalum ya mashindano yao.

Aidha Masudi ameeleza kuwa kanuni hizo watazipeleka kwenye chama cha mpira wa miguu Zanzibar ZFA ili kufanyiwa marekibisho kabla ya mkutano mkuu wa wajumbe wa ZAHLIFE kujadili kununi hizo.

‘’pia tunatarajia kuona michezo yetu ya ndani yote ya vyuo washindi wanakwenda kuwakilisha kwenye mashindano mbali mbali nje ya Zanzibar ikiwemo sanaa,mpira wa miguu,riadha na mashindano mengine ili kutengeneza nafasi za ajira za michezo kupitia wanavyuo’’ Alisema Masudi Juma.

Aidha mwisho amesema kwa sasa baada ya kutambuliwa rasmi kwenye rasimu ya katiba mpya ya ZFA kama wanachama mshiriki wa ZFA hivyo wanatakiwa wawe na kalenda ambayo ZFA wataitaumbua na kanuni zao kuwa bora zaidi.