Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amesema kuwa Zalio la vyeti feki ni Chama cha Mapinduzi na Serikali yake.

Halima Mdee ametoka kauli hiyo bungeni Mjini Dodoma, leo Mei 23, 2018 na kusema kuwa kuna walimu au watumishi wamelitumikia taifa hili kwa miaka mingi sana, serikali inadhani ni sahihi kwa watumishi hao kuondoka bila hata kifuta jasho?

“Zalio la vyeti feki ni Chama cha Mapinduzi na Serikali yake, kwa kipindi hicho tunafahamu kwamba walimu au watumishi wengi walianza na cheti cha mtu wakaenda wakasomea taaluma wakafaulu taaluma zao wakaenda kulitumikia Taifa hili kwa miaka mingi sana, serikali ya watu ni serikali yenye ubinadam mi nataka niulize swali la nyongeza hivi kweli serikali ya CCM inadhani ni sahihi kwa watu ambao wametumikia hili Taifa kwa miaka 20 wengine mpaka miaka 40 wengine hata miaka 30 waondoke hivi hivi bila hata kifuta jasho mnadhani ni sahihi.? amehoji Mdee.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Madini,Angellah Kairuki akijibu kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI amesema kuwa “Nafahamu kuwa dada/Mdogo wangu naye ni mwanasheria ‘You can make benefit for your own wrong’ suala hili lilikuwa ni jinai huwezi ukanufaika hata kama uliweza kupenetrate katika mfumo ikafikiwa hapo na Ndio maana Mh. Rais aliweza kutoa armnest na hii haikuweza kutoka bure, kwahiyo Mh. Halima aweze kuelewa suala hili halijazalishwa na serikali ya CCM ni criminal offence na ilikuwa ni lazima kufanya hivyo.”