Mwakilishi wa kuteuliwa na Rais Ahmada Abdulwakiil Shaa ameitaka Jamii kupendana na kusaidiana katika masuala mbalimbali ili kuendeleza Utamaduni na Silka za Mzanzibar.

Ameyasema hayo huko kwa Mchina Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ wakati alipokuwa akikabidhi msaada wa vyakula kwa wafanya kazi wake na watu wasiojiweza.

Amesema Zanzibar imepata heshima kubwa ndani na nje ya nchi kutokana na Wananchi wake kuwa  na ukarimu na Uzalendo hivyo kunauhitaji kuendelezwa kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Aidha amewaomba Wenye uwezo kuwasaidia wasiojiweza ili waweze kukabiliana na hali ngumu ya maisha walionayo katika familia zao.

Miongoni mwa vitu vilivyotolewa ni pamoja na Mchele, Sukari, Sabuni na mafuta ya kupikia ili waweze kujikimu katika kipindi cha Skuu ya Idilfitri.

STORY NA TAKDIR ALI