Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika harakati za kukabiliana na vurugu za walevi, imewasilisha muswada unaolenga kuipa nguvu zaidi Sheria ya Vileo ya mwaka 1928 ili kudhibiti ulevi nchini.

Muswada huo ambao tayari umewasilishwa katika Baraza la Wawakilishi utaweka masharti ya kuzuia, kudhibiti na kusimamia uagizaji, uhifadhi kwenye maghala, uuzaji, usambazaji na unywaji wa vileo

Vilevile, Muswada huo unazuia mtu, idara ya Serikali au taasisi yoyote kuuza au kutunza vileo vinavyochochea ulevi bila kuwa na leseni

Watakaokiuka Sheria na kukutwa na hatia watahukumiwa kifungo cha miaka isiyopungua mitano au kulipa faini isiyopungua Milioni 5