Mtendaji Mkuu
Zanzibar24 Nd.Suleiman Juma Is-haka
Akitoa shukrani za dhati kuhusiana na ushindi walioupata

Uongozi wa chombo kinachorusha Habari Mitandaoni Zanzibar24 leo April 25-2019 kimeipongeza Mamlaka ya kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar kwa kuwapatia ushindi wa Makala na habari mbali mbali zinazohusiana na Rushwa na Uhujumu Uchumi ambapo Muandishi wao Tatu Juma ameshika nafasi ya pili katika mvutano wa uandishi wa Habari za TV.

Akitoa shukrani za dhati kwa niaba ya timu nzima Mtendaji Mkuu
Zanzibar24 Nd.Suleiman Juma Is-haka amesema wameipongeza Mamlaka ya kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi ZAECA kwa kutambua ufanisi pamoja na mchango mkubwa kwa waandishi wa Habari na kuamua kueka zoezi hilo.

Pia amempongeza Muhariri wao Tatu Juma ambae ndie aliechukua uchindi Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi ZAECA amesema“Sisi hii kwetu imekua sio tunzo tu bali imekuwa ni hamasa iliyotuonyesha kwamba sisi tunaweza na kutufungulia njia na milango katika kuendeleza kazi zetu zenye ubora”

Hata hivyo Suleiman Ametoa rai kwa Mamlaka nyengine pamoja na Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya kale wajenge tabia kama hiyo yakufanya mashindano mbali mbali kwa Waandishi kwani itawasaidia vijana ambao wanajitolea kufanya kazi kubwa Zanzibar.

Wale ambao wanajitolea katika nchi vinapokuja vitu kama hivi inakuwa kwao ni jambo kubwa sana kwani ni historia ambayo haitofutika. amesema Suleiman