Zari amjia juu Diamond mwenendo wa malezi ya watoto wake

Zari The Bossy aja juu kuhusu msanii Diamond Platinumz suala zima la malezi ya malezi kwa watoto wake.

Mwana dada huyo ambaye ameachana na Diamond kwa muda mrefu sasa na kuamua kukaa na watoto wake aliowapata na msanii huyo anasema kuwa anamshangaa sana Diamond kwa kitendo cha kukubali kutumia muda wake mwingi kwa ajili ya kufanya starehe na sio kuwajali na kuwa karibu na watoto wake mpaka anasaidiwa na wanaume wenzake.

“too bad your kids will have all this  beautiful memories with somebody else..the simple things money cant buy.”aliandika kwenye ukuraza wake.

Hata kama amekuwa akionekana yuko afrika ya kusini akiwa na watoto hao, kwa mujibu wa zari anaona kuwa watoto hao hawapati muda mzuri na wa kutosha kukaa na baba yao hivyo wamekua wakipewa mapenzi ya baba  na watu wengine.

Lakini pia Zari anasema kuwa pamoja na kwamba Diamond amekua na pesa lakini kuna vitu haviwezi kununuliwa kwa pesa ikiwepo hilo.