Zari akitangaza uhusiano wake mpya katika mtandao huo wa kijamii siku ya Ijumaa jioni, Zari Hassan alisema kuwa mpenzi wake mpya amemkubali yeye pamoja na watoto wake wote watano kwani Mpenzi huyo mpya ambaye amemtaja kuwa Bwana ‘M’ katika mtandao wake wa Instagram ndiye aliyechukua mahala pake Diamond.

“Kwako wewe mpenzi nimejifunza mengi; Nakumbatia maisha yalivyo kwa sababu ya unyenyekevu wako. Nimekuwa nikifikiria maisha yangu ya baadaye lakini sikuweza kujua maisha hayo yatakuwa vipi. Watoto watano, wanaume wengine lakini bado ukaniona mimi kuwa mwanamke mrembo zaidi”, alisema Zari katika chapisho lake ambalo limevutia majibu 100,000.

”Nakupenda sana bwana M, na sio vitu vyenye thamani unavyonionyesha, nimeviona hivyo na hata vikuu na vizuri zaidi. Lakini ni wewe, moyo wako, uwepo wako na vile unavyotufanya mimi na wanangu kukuhisi. Wewe ni jasiri sana bwana M: Watoto watano ; mimi mwenyewe nina umri wa miaka 38…wow…umetumwa kutoka mbinguni mpenzi. Nakupenda bwana M”,aliongezea Zari katika chapisho hilo.

Zari Hassan alilaumu uzinzi na ukosefu wa heshima kama kitu kilichomshinikiza kujitenga na Diamond.

Hata hivyo Diamond aliamua kuendelea na maisha yake na mtangazaji wa Kenya tanasha Oketch ambaye ameapa kufunga ndoa naye.

Zari Hassan ana watoto wawili na Diamond na wengine watatu na mumewe wa zamani marehemu Ivan Ssemwanga.