ZFA yawafyekelea mbali waamuzi waliochezesha Jang’ombe Boys dhidi ya KMKM

Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) imewafungia Waamuzi wawili walio chezesha mchezo nambari 43wa ligi Kuu  ya Zanzibar, Jang’ombe Boys dhidi ya KMKM jumapili ilopita  kwa muda wa Mwezi mmoja.

Waamuzi hao ni Muamuzi wa kati Ali Ramadhan Ibada (kibo) na Muamuzi msaidizi Mustafa Hasira wamefungiwa baada ya kushindwa kuzitafsiri vyema Sheria 17 za Soka hususan sheria namba 11 ya mpira wa kuotea (Offside) katika mchezo uliochezwa juzi katika uwanja wa Amani ambapo Jang’ombe Boys wakatoka sare ya 1-1 dhidi ya KMKM.

Kwa mujibu wa Msemaji wa ZFA Abubakar Khatib Kisandu  amesema wamewafungia waamuzi hao mwezi mmoja huku akitoa onyo kali kwa waamuzi wengine waamuzi hao wamefungiwa kuanzia Novemba 6 hadi Disemba 5 kwa mujibu wa kanuni ya 15(9) (e) ya ZFA.

Aidha Kisandu amesema wao ZFA hawatamfumbia macho mwamuzi yeyote atakae enda kinyume na kanuni na taratibu za mpira wa miguu zinavyotaka.