Shirikisho la mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) kwa kushirikiana na shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wameandaa kozi maalum ya siku nne 4 ya masuala ya Tiba ya viungo.

Shirikisho hilo linatarajia kuendesha kozi tatu ikiwemo kozi ya magolikipa, kozi ya madaktari wa michezo na kozi ya uongozi, Mafunzo hayo yanatarijiwa kufanyika katika uwanja wa Mau kati kati ya mwezi wa nane mwaka huu.


Mkufunzi was kozi hio anatarajiwa kuwa ni Johnny Wilson kutoka U.K na kozi inaaanza August 17 Hadi 20 mwaka huu katika viwanja vya Mau.