Shirikisho la Soka Visiwani Zanzibar (ZFF) limefuta kadi zote za adhabu kwa wachezaji waliooneshwa wakati ligi kuu ilipochezwa awali na sasa kuanzia kesho watacheza wakiwa safi isipokua mchezaji/wachezaji ambao watapata kadi zitaanza kuhesabiwa tena upya.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho July 1, 2020 kwa kuchezwa michezo minne katika Uwanja wa Mao Kisiwani Unguja na katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.

Katika uwanja wa Gombani saa 8:00 mchana Selem View wataanza na Mafunzo kisha saa 10:00 jioni kiwanjani hapo Jamhuri watakipiga na timu ya Polisi.

Na katika uwanja wa Mao A Kesho saa 10:00 za jioni Zimamoto watacheza na Mlandege, muda huo huo katika uwanja wa Mao B JKU watakipiga na Kipanga.

Bingwa wa Ligi hiyo atapata nafasi ya kuiwakilisha Zanzibar kwenye Mashindano ya kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika.

Story by www.dimbani.co.tz