Zimamoto ipotayari kutoa elimu kwa mtu mmoja mmoja

Kitengo cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar KZU kimesema kipotayari kutoa elimu bure kwa kupitia shehiya za vijiji kwa mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu juu ya kujikinga na majanga ya moto.

Kauli hiyo imetolewa na  Naibu Kamishna wa Zimamoto na Uokozi Zanzibar Gora Haji Gora wakati akizungumza na Zanzibar24.

Amesema chanzo cha matukio mengi ya moto  ni Matumizi mabaya ya umeme hivyo ameishauri jamii kuhakikisha wanazima vifaa vya umeme baada ya matumizi na kufuata taratibu za kutumia majiko ya gesi majumbani kwao.