Timu ya Zimamomoto inayoshiriki Ligi kuu Zanzibar imeing’oa timu ya Kmkm ambayo ilikua inashikilia nafasi ya pili na sasa Zimamoto imeikamata nafasi hiyo ikitokea nafasi ya tatu.

Ikiwa tayari takribani michezo 192 na magoli 375 yameshafungwa katika msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar .

Ligi hio leo itaendelea tena kwa kuchezwa michezo mitatu kwa Unguja na Pemba .

Mchezo wa kwanza utachezwa Saa 8:00 kati ya Selem View na Cipukizi katika uwanja wa Gombani Pemba.

Mechi nyengine itapigwa Saa10 Jamhuri na Mwenge katika uwanja wa Gombani Pemba nao Mlandege watashuka Dimbani mbele ya Mafunzo katika uwanja wa Mao A Saa 10 :00 Jioni.

Story by www.dimbani.co.tz