Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam akitokea Kituo cha Polisi Mburahati mchana huu nakusomewa mashtaka yake.
Zitto amesomewa mashtaka 3 ya kutoa maneno ya uchochezi yenye nia ya kuleta chuki kwa Watanzania dhidi ya Jeshi la Polisi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Zitto amekana makosa amesema si kweli na ameachiwa kwa masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja, kusaini bondi ya Milioni 10. Kesi imeahirishwa hadi November 26,2018.