Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Zubeir Kabwe amedai kuwa picha ya gari inayosadikika kumteka Mo Dewji iliyooneshwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro haijapigwa eneo la tukio.

Zitto Kabwe ameeandika kupitia ukurasa wake wa Twitter muda mfupi baada ya Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro kutoa taarifa rasmi ya kuona gari iliyotumika kumtekea bilonea wa Afrika mashariki Mo Dewji kwa kumaanisha  kuwa taratibu zinazotumika kupiga picha gari zinatia mashaka makubwa.

“Hawa Polisi @tanpol wanadhani kila Mtanzania ni zwazwa anaweza kudanganywa danganywa tu. Taratibu za gari kupita mpakani zinatia mashaka makubwa kauli ya IGP. Polisi na vyombo vya usalama nchini hutumia plate number za Kigeni. Ile picha ya gari sio ya CCTV. Kamanda Sirro HAPANA”