Taarifa Rasmi: Z.M.A kusitisha safari za baharini kutokana na upepo

Mamlaka ya usafiri baharini (ZMA) inawatangazia wamiliki na watumiaji wa vyombo vyote vya baharini kusitisha shughuli zote zinazotumia njia ya bahari kutokana na upepo mkali ulioanza Jana Oktoba 22, 2018.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri baharini Abdalla Husein Kombo.

Mamlaka inawaomba kuwa wastahamilivu hadi hapo hali ya hewa itakaporejea katika hali yake ya kawaida.