Afisa uhusiano kutoka ZRB Makame Khamis

Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) imesema itahakikisha inaendelea na utaratibu wa kutoa elimu ya kodi kwa wananchi wa rika zote ili kuengeza kasi ya upatikanaji wa mapato za Serikali.
   

Akizungumza na Wanafunzi wa skuli ya Sekondari ya Nungwi katika mafunzo ya siku moja juu ya Ulipaji kodi na umuhimu wa kudai risiti Afisa uhusiano wa Bodi ya mapato Zanzibar (ZRB) Makame amesema kuna baadhi ya watu hawana elimu ya kutosha juu ya masuala ya ulipaji kodi na kusababisha kupoteza mapato ya serikali na wengine kukosa haki zao wakati wa ununuzi wa bidha ikiwemo kutopewa risiti ya uhalali wa bidhaa alizonunua.             

Amesema kila mwananchi anapaswa kupewa risiti kwa bidhaa anazonunua ili kuiwezesha serikali kufikia malengo waliyo yakusudia katika ukusanyaji wa mapato.
     

Akiwasilisha mada juu ya Umuhimu wa kulipa kodi,Afisa Elimu kwa walipa kodi Raya Suleiman Abdallah amewataka wananchi kuthamini juhudi za serikali kwa kuendeleza masharikiano ya kulipa kodi bila shuruti.          

Amesema wananchi watakapo lipa kodi ipasavyo na kudai risiti itaweza kuimarisha vyanzo vya mapato ya serikali kwa lengo kuengeza upatikaji wa huduma muhimu ikiwemo maji safi na salama pamoja na kuiwezesha miradi ya maendeleo kumalizika kwa wakati.
     

Aidha amewataka  Wanafunzi hao kuwa walimu katika jamii na familia zao juu ya kuwahimiza umuhimu wa kulipa kodi pamoja na kudai risiti ili kuchangia upatikaji wa huduma muhimu.
     

Kwa upande wao wanafunzi walioshiriki mafunzo hayo wamesema ni vizuri kuona taasisi za serikali zinajuwa umuhimu wa mafuzo ya ziada kwa wananfunzi jambo ambalo linawajengea uwezo wa kujua haki zao katika jamii.      

Akizungumza kwa niaba ya  wanafunzi hao Raisi wa Skuli ya Sekondari Nungwi Muhsin Hassan Ali  amesema watahakikisha wanatumia vyema mafunzo hayo ili kuiwezesha ZRB kukusanya mapato ipasavyo.
     

Aidha wamewataka wafanya kazi wa ZRB kutowavumilia baadhi ya wafanya kazi wanaokiuka sheria za ukusanyaji wa kodi ikiwemo kuwasamehe kodi watu wanaojuana nao ili kuzuia mapato ya Serikali yasipotee.

Na;Fat-hiya Shehe Zanzibar24