Afisa Uhusiano wa Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB Makame Khamis Muhammed

Afisa Uhusiano wa Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB Makame Khamis Muhammed amesema kila mwananchi anajukumua la kulipa kodi ili kuchangia ukuwaji wa maendeleo ya Nchi.

Akizungumza na Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Tumbatu katika Mafunzo ya siku moja juu Umuhimu wa kulipa kodi Afisa Makame amesema baadhi ya jamii bado haina uelewa juu ya umuhimu wa kulipa kodi ipasavyo jambo ambalo linasababisha kupotea kwa baadhi ya mapato ya serikali.      

Amesema lengo la kutoa elimu katika Kisiwa hicho ni muendelezo wa Utaratibu wao wa kutoa elimu ya mlipa kodi kwa  wananchi wote wa Zanzibar ili kuengeza ukuwaji wa ukusanyaji mapato.


Hata hivyo amefahamisha kuwa Wanafunzi ni Wawakilishi wazuri kwa Familia hivyo wakipatiwa elimu hiyo wataweza kuisaidia serikali kufikia malengo waliyo yakusudiwa katika kutoa huduma bora kwa jamii pamoja na kuiwezesha Miradi ya Serikali. kumalizika kwa wakati na kuleta Tija kwa wananchi.   

Wakitowa michango kwa Niaba ya Wanafunzi walioshiriki mafunzo hayo  Haji Twalib na Mwanahawa Kombo wameipongeza ZRB kwa kuamua kuwafikia katika kisiwa chao juu ya kuwafunza umuhimu wa kulipa Kodi.

Wamesema taasisi nyingi za Serikali haziwafikii katika kijiji chao jambo ambalo linawakosesha fursa ya kupata elimu ya Ziada itakayosaidia kuimarisha ukuwaji wa Uchumi Nchini.

Aidha wameahidi kuyafanyia kazi mafunzo waliyoyapata kwa kuwafunza wengine ili kuiwezesha serikali kunufaika na vyanzo vya Mapato vya ndani ya Nchini.          

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Skuli ya Secondar ya Tumbatu Makame Khamis Nyange amezitaka Tasisi za Serikali na Binafsi kujitolea katika kuwapa elimu ya ziada Wanafunzi wa Skuli hiyo ili kuwajengea uwezo wanafunzi wanapomaliza masomo yao.


Mwalimu Makame amesema Mwanafunzi anahitaji Elimu ya Skuli na ya kijamii ili kuweza kuwa raia mwema baada ya kumaliza Elimu ya Secondary.

Amesema wakati umefika kwa Tasisi za Serikali kufuata Utaratibu wa ZRB katika kutoa elimu ya kwa wanafunzi wa Mikoa yote ya Zanzibar ili waweze kujua wajibu wao wanapomaliza elimu yao ya Sekondari.

Wanafunzi Kisiwani Tumbatu wakiwa katika mafunzo ya siku moja juu Umuhimu wa kulipa kodi.

Hii ni mara ya Kwanza kwa Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB kufanya Safari ya Kutoa Elimu ya Mlipa kodi katika Wilaya ndogo ya Tumbatu ambayo kisiwa chake kipo pembezoni mwa Wilaya za zanzibar.     

Na:Fat-hiya Shehe Zanzibar24