Mkurungenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar(ZSSF) Bi. Sabra Issa Machano ameeleza sababu za kuchelewa kwa mradi wa Michenzani Mall ambao ulipangwa kumaliza June 2020.

Akieleza hayo kupitia ukurusa wake Instagram Bi Sabra amesema

”Tuliahidi kumaliza June 2020 lakini Covid 19 na kufungwa kwa mipaka ya dunia kumechelewesha kufika kwa vifaa vingi. Inshallah tunategemea mradi wetu utakamilika mwanzoni mwa August 2020”

“Wakati maisha yetu yamegubikwa na wasiwasi wa maradhi ya corona, Rais wetu ametutaka tuendelee na kazi na sisi ZSSF tunatekeleza. Tukiahidi tunamaanisha ila sisi tunapanga yetu na Mungu anapanga yake. Ila tunajitahidi kutekeleza matumaini ya Wadau wetu” 

Oktoba 4, 2018 ZSSF walitiliana saini na kampuni ya Ujenzi ya CRJE kwa ujenzi wa jengo hilo ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya ZSSF Dkt. Suleiman Rashid Mohammed alisema Mradi huu unatarajiwa kumaliza ifikapo June 2020.