Mfuko wa hifadhi ya wa jamii Zanzikbar ZSSF imeichangia shiling milioni 5 Timu ya Taifa ya Zanzibar  “Zanzibar Heroes’   ili kuunga mkono timu hio ambyo ipo nchini Uganda kwa mashindano ya Cecafa.

Hayo yamesemwa na afisa uhusiano wa ZSSF ndugu. Juma Mmanga wakati akikabidhi cheki hio kwa rais wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) huko katika ofisi za ZFF Amani Mjini zanzibar.

“Tuna paswa kuwaunga mkono vijana wetu katika soka kwani kufanya hivyo kutapelekea kuwapahamasi zaidi ya kufanya vizuri kwani wanafanya kazi nzuri ya kuipeperusha bendera ya Zanzibar kimataifa”. Amesema Mmanga

Nae Rais wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) Seif Kombo Pandu  amesema anaishukuru sana ZSSF kwa kuwaunga mkono pamoja na kuwajali kwani fedha hizo zitasaidia kutatuwa changamoto zinazoikabili timu hiyo.

Aidha amewataka wadau wengine kuendelea kujitokeza katika kuichangia timu hio ya nyumbani ili kuweza kufikia malengo kwa vijana wa Zanzibar.