Wafanya kazi nchini wametakiwa kuhamasishana na kujiunga katika mfuko wa hifadhi ya jamii ZSSF ili waweze kujisaidia na kujikwamua na hali ngumu ya kimaisha pindipo wanapofikia umri wa kustaafu

Wito huo umetolewa na waziri wa katiba na sheria Mhe.Khamis Juma Mwalimu katika hafla ya ufunguzi wa mkutano wa tano wa wadau  wa ZSSF uliofanyika huko kwenye ukumbi wa Uhuru kariako Mjiniz Zanzibar

Amesema kuwa “wafanyakazi wengi hawana muamko wa kujiunga katika mfuko jambo ambalo linawafanya kukosa mafao yatakayo wasaidia wakati wa kustaafu” hivyo kuwashauri wafanya kazi wa ZSSF kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujiunga na mfuko huo wafaidike

Aidha Mh.Khamis amekadhi zawadi zawadi kwa wachangiaji bora wa mfuko mkuu na wa ZVSSS na kwa wafanyakazi bora wa tasisi hio

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ZSSF Bi sabra Issa Machano  amewataka wafanya biashara kujiunga na mfuko wa hiyari ambao una mafao ya muda mfupi na muda mrefu

Kauli mbiu ya mkutano huo wa tano wa washirika wa zssf kwa mwaka huu ni “mikataba ya kazi ni nguzo ya wanachama wa ZSSF”