Licha ya wastaafu mbalimbali kufika katika maeneo ya Mjini kuhakiki taarifa zao Mfuko wa hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF imesogeza huduma hizo karibu kwa wanachama wake ili kuondoka usumbufu wa kufata huduma hizo mjini.

Hayo yameelezwa na afisa habari na masoko muandamizi  ZSSF Bi Raya Hamdani Khamis huko katika Ukumbi wa T-C Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja katika muendelezo wa zoezi la uhakiki kwa wastaafu wa mfuko huo.

Amesema wastaafu wengi wamekuwa wakihakiki taarifa zao mjini licha ya kuwa huduma hizo zimezogezwa karibu na maeneo yao wanayoishi.

Akitolea ufafanuzi kuhusu wazee wagonjwa Bi Raya amesema ZSSF imekuwa ikiwafata wastaafu hao majumbani kwako ili nao wajihakiki taarufa zao.

Akizungumza Mara baada ya kuhakiki taarifa zake mzee Suleiman Kaibu Vuai ameuomba uongozi wa ZSSF kuongeza posho kwa watu wastaafu wa muda mrefu ili kujikimu kimaisha.

Zoezi Hilo kwa Wilaya ya Kati litaendelea kwa siku tutu ikiwa ni muendelezo wa uhakiki kwa wastaafu wanaopokea pencheni zao Mfuko wa hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF kuhakiki taarifa zao ambapo jumla ya wastaafu 11,100 wanatarajiwa kuhakikiwa taarifa zao katika vituo mbalimbali kote.