ZURA: Hali halisi ya mafuta Z’bar October 15, 2018

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) inapenda kutoa Taarifa kwa Wananchi juu ya hali halisi ya mafuta nchini.

Hali halisi ya uwepo kwa mafuta hapa nchini hadi siku ya Jumatatu tarehe 15 October, 2018 inaonyesha ya kwamnba kwa upende wa kisiwa cha Unguja kuna mafuta kiasi cha lita 1,884,220 ya petrol yanayoweza kutumika kwa muda wasiku kumi na mbili na mafuta ya Dizeli lita 2,031,120 yanayoweza kutumika kwa muda wasiku kumi na tatu na mafuta ya taa lita 501,148 yanayoweza kutumika kwa mud wasiku 10.

Kwa upande wa pemba hadi siku ya Jumatatu tarehe 15 October, 2018 kuna mafuta kiasi cha lita 232,075 za petrol ambazo zinaweza kutumika kwa muda wa siku sita, lita 195,174 za dizeli zinazoweza kutumika kwa muda wa siku 30 .

Aidha meli ya united sprit inatarajiwa kupokea lita 2,047,500 za mafuta ya Petroli, na dizeli lita 1,800,000 ya mafuta  kuanzia siku ya Jumamosi  ya tarehe 11 Octoba 2018 yanayo tarajiwa kutumika kwa muda wa wiki mbili.